NEWS

30 Aprili 2019

JPM Atoboa SIRI ya Mwakyembe Kutaka Kuuawa kwa Sumu

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Rais John Magufuli ametoboa siri ya Mbunge wa Kyela ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa uzalendo wake wakusimamia haki ndiyo uliyosababisha watu wenye nia ovu kumnywesha sumu na kwenda kutibiwa nje ya nchi.

 

Rais meyasema hayo leo Aprili 30, 2019 wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kyela mkoani Mbeya katika mkutano wa hadhara ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi kwa siku nane mkoani humo.

 

“Dkt. Mwakyembe alikuwa Naibu Waziri wangu alinisumbua sana, amewahi kunyweshwa sumu akapelekwa nje kwa sababu ya kusimamia haki, inawezekana nyinyi watu wa Kyela hamumjui Mwakyembe, mimi namfahamu vizuri,” alisema Magufuli ambapo pia aliendelea na kugusia siala la vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.

 

Alizitaka mamlaka husika kutowatoza chochote wenye vitambulisho, badala yake washughulike na wasio na vitambulisho, kwani wenye vitambulisho  wameshachangia  shilingi elfu ishirini kwa mwaka mzima kwa kununua vitambulisho hivyo.

 

Alisema serikali imeboresha kilimo kwa kutoa mikopo, hadi mwezi Machi 2019, ambapo sh.. Bil. 102 zilitolewa kwa wakulima na wakulima wa Mbeya wamekopa sh. mil. 799 tu, hivyo akatoa wito ili wakope kwa ajili ya kilimo.

 

Pia alisifia uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Malawi na kuwataka Watanzania wafanye biashara na nchi hiyo jiranina akazungumzia pia jitihada za serikali yake katika kuimarisha usafiri wa anga kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi.

 

“Tunataka maparachichi yawe yanabebwa na ndege yanakwenda moja kwa moja Ulaya, tunafanya hivi kwa ajili ya wananchi wanyonge,” alisema akisitiza juu ya umuhimu kiuchumi kwa Watanzania wote katika ununuzi wa ndege, hali ambayo imeweza kuifanya serikali yake kumudu gharama mbalimbali za utoaji huduma ikiwa ni pamoja na kutolewa kwa Sh. bilioni  23.86 katika sekta ya elimu na mishahara kwa wafanyakazi kila mwezi.

 

VIDEO: MSIKIE MAGUFULI AKIZUNGUMZA

The post JPM Atoboa SIRI ya Mwakyembe Kutaka Kuuawa kwa Sumu appeared first on Global Publishers.