NEWS

29 Aprili 2019

Mavazi yanayofunika uso marufuku Sri lanka

 

Sri Lanka imepiga marufuku watu kujifunika uso hadharani kufuatia mashambulio ya kujitoa mhanga katika sikukuu ya Pasaka yaliosababisha vifo vya watu zaidi ya 250 na mamia wengine kujeruhiwa.

 

Rais Maithripala Sirisena amesema anatumia sheria ya dharura kuidhinisha marufuku hiyo kuanzia leo Jumatatu na amesema ameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha usalama wa raia wa nchi hiyo dhidi ya ugaidi.

 

Sri Lanka inasalia kuwa katika tahadhari kubwa siku nane baada ya mashambulio makubwa yanayoelezwa kutekelezwa na itikadi kali za dini ya kiislamu dhidi ya makanisa na hoteli nchini humo.

The post Mavazi yanayofunika uso marufuku Sri lanka appeared first on Global Publishers.