NEWS

30 Aprili 2019

Mbunge Ahoji Tulia Kuongozana na Magufuli


Mbunge wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msiwa (CHADEMA) amehoji ni kwa nini Naibu Spika Tulia Ackson ameondoka bungeni na kwenda kujiunga kwenye ziara ya Rais Magufuli inayoendelea huko Mbeya.



Mch. Msigwa amehoji hayo leo ikiwa ni siku ya tano ya ziara ya Rais Magufuli ndani ya Jiji la Mbeya ambapo awali ilielezwa kuwa itakuwa ziara ya siku nane ya kikazi.

"Ameacha Bunge linaendelea, yeye ni mhimili mwingine anafuata fuata nini huko kwenye mhimili wa serikali"?, amehoji Msigwa.

Katika kukazia hoja yake, Msigwa ameongeza kuwa, "yeye sio Mbunge wa mbeya, aliapa Kinondoni na alipiga kura huko".

Hata hivyo, harakati za Naibu Spika ndani ya Jiji la Mbeya zimekuwa zikihusishwa na kuwania kiti cha ubunge kwa jimbo la Mbeya Mjini kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020.