NEWS

17 Aprili 2019

Omar al-Bashiri apelekwa Gerezani

Rais aliyeondolewa kwa nguvu madarakani nchini Sudan Omar al-Bashir amehamishiwa katika jela ya Kobar iliyopo kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum. Taarifa hiyo imetolewa na familia ya Bashir

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Bashir alikuwa akishikiliwa chini ya ulinzi mkali katika makaazi ya rais baada ya kuondolewa kwake madarakani na jeshi Aprili 11.

Wakati huohuo waandamanaji bado wanaendelea kupiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi wakitowa mwito wa kuundwa serikali ya kiraia na jeshi kujayakabidhi madaraka kwa amani.