NEWS

28 Aprili 2019

Video: Rais Magufuli Ashuhudia Kusimikwa Kwa Askofu Nyaisonga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Janeth Magufuli  leo wameshiriki Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu Mteule, Gervas Nyaisonga kuwa Askofu Mkuu wa kwanza  Jimbo Kuu Jipya la Mbeya. Ibada inafanyika katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Rais Magufuli yupo mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi ya siku nane.

Desemba 21 mwaka jana, Papa Francis alitangaza na kumteua Askofu Nyaisonga kuwa Askofu Mkuu wa kwanza Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya na kulitangaza kuwa Jimbo Kuu teule.

Awali, Askofu Nyaisonga alikuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda ambaye pia ni Rais wa  Baraza la Maaskofu  Tanzania (TEC).

The post Video: Rais Magufuli Ashuhudia Kusimikwa Kwa Askofu Nyaisonga appeared first on Global Publishers.