USIKU wa kuamkia leo Machi 31, 2019 kutangazwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora mwaka na Mfungaji Bora wa msimu katika hafla ya tuzo za MO Simba Awards 2019.
Kagere alishinda tuzo hiyo baada ya kuwapiku nahodha wa timu hiyo John Bocco na kiungo mshambuliaji Clatous Zambia anayetokea nchini Zambia.
Tuzo hizo mbili zimekuja siku chache baada ya Kagere kumaliza msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2018/2019 akiwa mfungaji Bora akipachika mabao 23, huku pia akishika nafasi ya pili kwa kufumania nyavu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na mabao sita.
Utoaji wa tuzo hizo ulianzia katika kipengele cha Kipa Bora wa mwaka ambayo mshindi kama ambavyo wengi walitegemea alikuwa ni Aishi Manula ambaye amedaka zaidi ya 90% ya mechi zote za timu hiyo msimu huu akimshinda Deogratias Munishi ‘Dida’ ambaye waliwania naye.
Tuzo hiyo ilitolewa na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Equity, Robert Kiboti na tuzo ambayo ilifuata ilikuwa ya Beki Bora iliyobebwa na Erasto Nyoni ambaye aliwashinda Pascal Wawa na Shomari Kapombe ambayo alikabidhiwa na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ubashiri wa matokeo ya michezo ya SportPesa, Pavel Slavkov.
Kipengele kingine katika tuzo hizo kilikuwa cha Kiungo Bora ambayo kiungo wa Ghana, James Kotei aliinyakua baada ya kuwashinda Mzamiru Yassin na Jonas Mkude.
Kama kuna kipengele ambacho kilionekana kingeleta ushindani mkubwa ni kile cha Mshambuliaji Bora wa klabu hiyo ambacho mshindi wake alikuwa ni nahodha John Bocco ambaye aliwashinda Emannuel Okwi na Meddie Kagere mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliomalizika.
Baada ya Bocco, kinda Rashid Juma alitwaa tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo wakati Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ambaye aliibuka mshindi wa kipengele cha mchezaji bora wa kike wa klabu hiyo.
Kulikuwa na tuzo ya Mchezaji wa wachezaji ambayo mshindi wake anapatikana baada ya kupigiwa kura na wenzake ambayo kwa mara nyingine ilienda kwa Erasto Nyoni na mshambuliaji Meddie Kagere alishinda tuzo ya Mfungaji Bora wa msimu.
Tuzo ya heshima ilikwenda kwa mdhamini wa zamani wa Simba, Azim Dewji ambayo ilifuatiwa na ile ya bao bora iliyokwenda kwa Clatous Chama kutokana na bao lake dhidi ya Nkana FC kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu unaomalizika.
Baada ya vipengele hivyo vyote kutajwa ndipo kikaja kile cha Mchezaji Bora wa msimu ambacho mshindi alikuwa ni Kagere.
LISTI NZIMA YA WASHINDI WA TUZO ZA
Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya Mo Simba 2019 ni Meddie Kagere.
Goli la Clatous Chama dhidi ya Nkana limeshinda Tuzo ya Goli Bora la Mwaka.
Tuzo ya Heshima inakwenda kwa Azim Dewji.
Meddie Kagere ameshinda Tuzo ya Mfungaji Bora wa Mwaka.
Erasto Nyoni ameshinda Tuzo ya Wachezaji.
Mwanahamisi Omary Shurua ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mwanamke wa Mwaka.
Rashid Juma ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka.
John Bocco ameshinda Tuzo ya Mshambuliaji Bora wa Mwaka.
James Kotei ameshinda Tuzo ya Kiungo Bora wa Mwaka.
Erasto Nyoni ameshinda Tuzo ya Beki Bora wa Mwaka.
Aishi Manula ameshinda Tuzo ya Golikipa Bora wa Mwaka.
The post Washindi wa Tuzo za Mo Simba Awards 2019 Wapo Hapa (Picha +Video) appeared first on Global Publishers.