INADAIWA kuwa beki wa Lipuli FC, Ally Mtoni ‘Sonso’ tayari amemalizana na uongozi wa Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara huku mwenye akifunguka kuwa ni kweli wapo kwenye mazungumzo.
Sonso ni mchezaji ambaye alikuwa akiwindwa na Yanga kwa muda mrefu tangu kipindi cha usajili wa dirisha dogo na ni mmoja kati ya wachezaji ambao waliipeleka Stars katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka huu.
Habari za ndani zinadai kuwa tayari nyota huyo amezungumza na kumalizana na Yanga baada ya mkataba wake na Lipuli FC kumalizika huku kukiwa hakuna mazungumzo yoyote na uongozi
Martha Mboma, Dar es Salaam huo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, mtu wa karibuni na nyota huyo alisema kuwa mambo ya nyota huyo na Yanga tayari yamefika pazuri kabisa na huenda msimu ujao akavaa uzi wa njano na kijani.
“Taarifa ambazo ninazo mpaka sasa ni kwamba Sonso tayari wamemalizana na Yanga na huenda msimu ujao akawa hapo kama mambo yao yataenda hivyo hadi mwisho. Gazeti hili lilimtafuta Sonso ambaye alisema:
“Ni kweli niko kwenye mazungumzo na Yanga na yanaendelea ila bado sijasaini lakini kila kitu kitawekwa wazi karibuni. Kwa sasa nipo Mtwara kwenye mechi ya FA.”
The post Beki Lipuli Mambo Safi Yanga appeared first on Global Publishers.