RAIS wa Klabu ya Real Valladolid, Ronaldo Nazario de Lima, amemsifia mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe na kusema kuwa anavutiwa na aina ya uchezaji wake. Nguli huyo wa zamani wa Real Madrid na Barcelona, ametoa kauli hiyo wakati presha ya Madrid kutaka
kumsajili Mbappe ikiwa kubwa wakati huu.
UNAISHI VIPI MAISHA YA KUWA RAIS WA KLABU?
Wakati wa mchezo napenda kujificha kwa kuwa taswira yangu inaweza kuwavuruga wachezaji na kuvivutia vyombo vya habari.
KWA NINI UMEAMUA KUWA RAIS NA SIYO KOCHA?
Sijawahi kutamani kuwa kocha, hata
wanaosomea ukocha wanapitia njia ngumu kuliko wachezaji, ndoto yangu ilikuwa kununua klabu Ulaya.
UWEPO WAKO HAPA UMEKUWA NA HAMASA YOYOTE?
Ndiyo, hilo limeonekana japokuwa wanasubiri kuona nitakachokifanya.
NI RAIS AU MMILIKI GANI ALIKUVUTIA?
Wapo watatu, Massimo Moratti (alikuwa Inter Milan), Florentino Perez (Real Madrid) na Andres Sanchez wa Corinthians. Nimekuwa na ukaribu zaidi na Florentino na amenifundisha vitu vingi. NI
RAHISI KUWA RAIS BILA KUSOMEA UKOCHA?
Inategemea, nimecheza soka na ninaujua mchezo lakini sitaki kuingilia kazi ya kocha wetu (Sergio Gonzalez). Sijaenda kwenye vyumba vya wachezaji na sitaki kufanya hivyo labda iwe kwa siku maalum.
NI NGUMU KWA KLABU KAMA VALLADOLID KUSHINDANA DHIDI YA TIMU KUBWA?
Ni ngumu lakini inawezekana, tulikuwa na bajeti ndogo lakini tumepambana. UNAKUBALI
WATU WANAOSEMA KUWA MBAPPE ANAFUATA NYAYO ZAKO?
Ndiyo nakubali, ninampenda. Ni mchezaji mwenye kasi na anaweza kufunga, umri wake ni miaka 20 tu lakini tayari tumeshamjua kwa miaka mitatu sasa, hiyo ni kwa kuwa ana kipaji cha hali ya juu.
UWEZO WA VINICIUS JUNIOR UMEKUSHANGAZA?
Hapana, nilimuona tangu akiwa Flamengo. Ana ubora wa juu na ndiyo maana Madrid walilipa euro 40m, bado hajakaa sawa lakini ni mchezaji mzuri na ataipa klabu mafanikio.
UNAIONAJE COPA AMERICA INAYOKUJA?
Tutakuwa nyumbani (Brazil) na kocha Tite ana wachezaji wazuri, tunatagemea mambo mazuri. Argentina wana Messi watakuwa wapinzani wetu wakubwa, pia kuna Uruguay, Chile nao ni hatari.
The post Ronaldo: Namkubali sana Mbappe appeared first on Global Publishers.