NEWS

31 Desemba 2019

VIDEO: “Moyo wa FARU Fausta ulifeli Akaanguka, Tunasherekea Kifo Chake”


Kwa mujibu wa taarifa ya upasuaji uliofanywa na jopo la Madaktari wa wanyamapori na wataalamu wengine wa uhifadhi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori nchini na Hifadhi ya Ngorongoro, wamesema Faru Fausta alifikwa na mauti, baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi vizuri.

Robert Fyumanga ni Daktari wa Wanyamapori, amesema kuwa kuta za moyo wa Faru Fausta, zilikuwa nyembamba sana hali iliyopelekea damu ishindwe kupita kwa ufasaha.

“Kuta za Moyo wake zimekuwa ni nyembamba sana hivyo kushindwa kusukuma damu ya kutosha mwilini, kwahiyo alikosa nguvu na kuanguka” Dkt. Fyumanga.

Faru jike mweusi ambaye alipewa jina la Fausta, ambaye pia ndiye Faru mzee kuliko wote duniani, alifariki dunia siku ya jana ya Disemba 28, 2019, katika eneo alilokuwa akihifadhiwa kutokana na maradhi ya uzee. VIDEO: