NEWS

23 Machi 2017

Nimeona Utupu wa Mke wa Mpangaji Mwenzangu..Sasa Imekuwa Tabu kwa Usumbufu Anaonipa..Ushauri Jamani Nifanyaje....!!!



Ilikuwa wiki moja iliyopita.Wakati wa asubuhi naingia bafuni kuoga kumbe kulikuwa na mke wa jirani yangu ambaye pengine hakusikia ujio wangu nami sikujua kama yumo.
  
Ile anataka kutoka tu pale mlangoni,kanga yake ikaanguka na akabaki mtupu Macho hayana pazia niliona utupu wake nae aliona kuwa nimeona.Ile tu anajizoazoa kujisitiri akateleza akaanguka ikabidi nimsaidie kumuinua , nikamwinua huku akiwa uchi wa myama na kuhakikisha hajaumia popote ...then nikamfunika na kumwambia pole nikaondoka kiistaarabu.
  
Ila sasa naona ustaarabu wangu uliniponza sasa naona ananifanyia vituko Mwanzo nilifikiri yameisha,alianza kwa kukwepesha macho na mimi,,mara akajenga mazoea na mimi.Na sasa vituko vimezidi,mara sms za ajab,wakati wote anataka kujua niko wapi na nafanya nini, siku ingine ananiletea chakula alichopika nile..
  
Kwa tabia na msimamo wangu naheshimu sana ndoa za watu.Nishaurini nifanye nini kumuepuka ? Nimepanga chumba hapa na nimelipa kodi ya mwaka mzima,ni jirani tu chumba cha nne toka kwangu...