NEWS

1 Juni 2019

Taifa Stars yapata jezi mpya Afcon – Video

sHiriKisHo la soka tanzania (tFF), jana limeingia mkataba rasmi na Kampuni ya romario sport 2010 Limited inayotengeneza jezi zenye nembo ya Uhlsport kwa ajili ya timu ya taifa ya tanzania, taifa stars.

 

TFF imeingia mkataba huo wa miaka mitatu na kampuni hiyo kwa lengo la kutengeneza jezi za timu zote za taifa ikiwemo Taifa Stars inayotarajia kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika ‘Afcon’ itakayofanyika Juni, mwaka huu nchini Misri.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, mara baada ya kuingia mkataba huo, Rais wa TFF, Wallace Karia alisema
kuwa, wameingia mkataba huo kutokana na kufanya vizuri kwaTaifa Stars kufuatia kufuzu kushiriki Afcon.

 

“Haya yote ni matunda ya Watanzania kufanya vizuri kwenye timu yetu ya taifa, tungekuwa tunafanya vibaya basi tusingeweza kupata mkataba huu maana kuna timu nyingi Afrika hazina mkataba wa kutengenezewa jezi.

 

“Lakini nichukue nafasi hii kuwaonya wale wote wanaotengeneza na kuuza jezi feki kwa kutumia nembo ya TFF, huu ndiyo mwisho wao kama watakuwa nazo basi waziuze haraka baada ya hapo hakutakuwa na kuangaliana usoni, tunataka kuona jezi hizi zikiwa tofauti na zile ambazo hazitambuliki,” alisema Karia.

 

Naye mwakilishi wa kampuni hiyo, Minhaal Dewji alisema kuwa, kwa upande wao wamejipanga kuzalisha jezi zenye ubora mkubwa ambazo zitakidhi gharama za Watanzania wote. Katika mkataba huo kutakuwa na ugawaji wa mipira 600 kwa timu zote za taifa huku zikitarajiwa kuzinduliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji wa Taifa Stars, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kabla ya Juni 7, mwaka huu kwenda Misri

The post Taifa Stars yapata jezi mpya Afcon – Video appeared first on Global Publishers.