GARI ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, jana lilipata ajali mbaya iliyosababishwa na mtoto wa dereva wake anayedaiwa ‘kuliiba’ na kutoka nalo. Imeelezwa kuwa deveva wa mkuu wa mkoa huyo na mkewe walizimia baada ya kusikia tukio hilo.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki, alisema tukio hilo limetokeo jana ambapo baada ya kuosha gari dereva huyo alifika nyumbani na hakulizima kwa kuwa alikuwa anatoka kumfuata mkuu wa mkoa. Alisema alivyoingia ndani dereva huyo alipata mgeni na kuzungumza naye.
“Wakati akizungumza na mgeni huyo mtoto wake mwenye umri wa miaka 24 alilichukua gari hilo bila ruhusa ya baba yake na kuondoka nalo.
“Alipofika eneo la kanisani lilimshinda na kuingia mtaroni. Hii ajali ni ya kizembe huyu kijana alikuwa spidi kubwa,” alisema RPC Ndaki na kuongeza kwamba madhara ni makubwa katika ajali hiyo kwani utengenezaji wake sio chini ya Sh milioni 80.
Aidha, alisema kijana huyo aliumia na kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
“Baba yake alipofika katika tukio hilo alizimia na mkewe alipopata habari za ajali hiyo naye alipoteza fahamu. Wote wamepelekwa hospitali,” alisema.
The post MTOTO WA DEREVA ANUSURIKA KIFO AKIENDESHA GARI LA SERIKALI appeared first on Global Publishers.