NEWS

29 Septemba 2019

Mbasha Apata Kigugumizi Penzi Lake na Muna

BAADA ya tetesi kusambaa kuwa anatoka kimapenzi na msanii wa Bongo Muvi, Rose Alphonce ‘Muna’, msanii wa nyimbo za Injili anayetikisa na wimbo wake wa Habari Njema, Emmanuel Mbasha amepata kigugumizi juu ya uhusiano wake huo.

 

Kwa mujibu wa chanzo, wawili hao wanadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda sasa na wamekuwa wakionekana pamoja maeneo mbalimbali pia kuonesha hisia zao hadi mitandaoni.

 

“Nyie hamjui tu, Mbasha na Muna mbona ni wapenzi wa muda mrefu tu. Ukiachilia mbali kuonekana baadhi ya sehemu, wamekuwa wakiwasiliana kama mtu na mpenzi wake na wakati mwingine hukutana na kushauriana,” kilisema chanzo na kuongeza;

“Ndiyo maana huwezi kushangaa, Mbasha akaingia kwenye ukurasa wa Instagram wa Muna na kujiachia kwa kumsifia au kumwambia maneno matamu yanayoashiria mtu na mpenziwe walioshibana,” kiliweka nukta chanzo hicho.

 

Baada ya madai hayo kusambaa, Risasi Jumamosi lilimtafuta Mbasha ili aweke wazi kuhusiana na mapenzi yao, baada ya kubanwa alipata kigugumizi na kuanza kucheka.

Risasi Jumamosi: Habari Mbasha, kuna madai yanasambaa kuwa unatoka kimapenzi na Muna?

Mbasha: Mmmmh nani kakwambia…hahahaha.

 

Risasi Jumamosi: Mbona unapata kigugumiza na hapohapo unacheka kulikoni?

Mbasha: Unanichekesha sana kwa kweli, mimi na Muna ni marafiki sana.. yaani yeye ananikubali nami namkubali sana.

Risasi Jumamosi: Kwa hiyo nyie ni wapenzi au siyo wapenzi?

 

Mbasha: (anacheka) bwana wewe kwani kuna mtu anateseka au anaumia Muna akiwa mpenzi wangu?

Risasi Jumamosi: Hakuna anayeteseka ila tunataka kuujua tu ukweli.

Mbasha: Muna ni rafiki yangu na hata hapa nipo naye tunakula wali na samaki aina ya sato.

Risasi Jumamosi: Je, una mpango wa kumuoa lini?

 

Mbasha: Kiukweli sina mpango wa kuoa leo wala kesho, nasubiri wakati wa Mungu ndiyo sahihi zaidi.

Awali Mbasha alikuwa mume wa ndoa wa mwimbaji wa Injili, Madam Flora (zamani Flora Mbasha) na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kike lakini ndoa hiyo ilivunjika na sasa Flora ameolewa, huku Mbasha akiwa bado yupoyupo kwanza.

STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi

The post Mbasha Apata Kigugumizi Penzi Lake na Muna appeared first on Global Publishers.