NEWS

1 Oktoba 2019

Kisa Mkwanja! Wananchi Kijiji Kizima Wameuza Figo Zao

JAMBO la kustaajabisha ambalo ninaamini hata wewe ungependa kufahamu kuhusu hili. Kijiji cha Hokse nchini Nepal kimebatizwa jina jipya la ‘Kidney Village’ kufuatia takribani watu wote wanaoishi kwenye kijiji hicho kuwa wameuza Figo zao.

Inadaiwa kuwa Wakazi wa Kijiji hicho hali zao za kiuchumi ni duni sana kitu kinachowasukuma kuingia katika biashara ya kuuza Figo zao ili wapate fedha za kujikimu mahitaji yao.

Mkazi mmoja aliyetambulika kwa jina la Geeta mwenye miaka 37 alisema kuwa yeye na Mume wake walisafiri mpaka kwenye Hospitali moja huko nchini India ili kutolewa Figo zao na kulipwa zaidi ya shilingi Milioni 3 za Kitanzania.

 

Aidha, familia hiyo ilitumia fedha hizo kununua kiwanja na kujenga nyumba yao na isivyo bahati nyumba hiyo iliangushwa na tetemeko la ardhi lililotokea kijijini hapo.

 

Kwa upande mwingine madalali wanaofanya biashara hiyo ya figo wametajwa kuzunguka sana katika kijiji hicho na kuwashawishi Wanakijiji hao kuuza Figo zao.

ITAKULIZA! MSANII AVUNJIKA MGONGO KIMAAJABU, ASIMULIA KILICHOTOKEA!

The post Kisa Mkwanja! Wananchi Kijiji Kizima Wameuza Figo Zao appeared first on Global Publishers.