NEWS

3 Oktoba 2019

Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Alivaa Gazeti Linalomchafua Mkewe, wafungua kesi


Watawala wa Sussex wamemaliza ziara yao ya siku kumi katika baadhi ya nchi za Afrika huku wakitangaza kufungua kesi dhidi ya gazeti moja la Uingereza la Sunday Mail ambalo nalo limesema litasimama ‘kidete’kujitetea dhidi ya kesi iliyofunguliwa na wanafamilia hao wa kifalme.

Leo Jumatano, mke wa mjukuu wa malkia wa Uingereza, Prince Harry, Meghan Markel ametangaza kufungua kesi dhidi ya gazeti hilo kwa madai ya kuchapisha taarifa ya barua yake binafsi aliyomuandikia baba yake, Thomas Markle kinyuma na sheria.

Kupitia waraka alioutoa, mtawala huyo wa Sussex amesema, hatua hizo za kisheria zinafanyika kama majibu ya kudhibiti “propanda zinazoendelea dhidi ya mke wake”.

Gazeti la Sunday Mail kupitia msemaji wake limesema linasimamia taarifa iliyoitoa na watajitetea mahakamani.

Prince Harry amesema "Mwitikio chanya" wa upashaji habari za wawili hao katika ziara yao Afrika imefichua “upendeleo wa wazi” wa "chombo hicho ambacho kimekuwa kikimdhalilisha [Meghan] karibia kila siku kwa kipindi cha miezi tisa".

Gazeti hilo linashutumiwa kwa kuandika "kuingilia na kuchapisha kinyume cha sheria barua binafsi" pamoja na kuendesha kampeni za kuchapisha taarifa za uongo na kumdhalilisha mke huyo wa mtawala wa Sussex