NEWS

20 Novemba 2019

Alichokisema Lema baada ya Meya wa CHADEMA Arusha kutimkia CCM


Baada ya aliyekuwa Meya wa Jiji la Arusha, Kalisti Lazaro kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ametoa neno.

Lema amesema kuwa ni baraka kubwa kwa Chadema Meya huyo kuondoka kwenye CCM huku akidai kuwa bado rafiki yake mmoja.

"Wakati Yesu Kristo anataseka msalabani Wayahudi walikuwa wanapiga kelele wakisema amekwisha,amekwisha..lakini yeye alisema Imekwisha," ameandika Lema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

"Wanafikiri tumekwisha na kumbe Imeisha. Ni baraka kubwa  kwa Chadema Mayor wa Arusha Mjini Kalist Lazaro kwenda CCM,bado rafiki yake mmoja."