NEWS

14 Novemba 2019

Balama Apagawa Na Mkwasa Yanga SC

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga ,Charles Mkwasa.

BAADA  ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Balama Mapinduzi ‘Penseli’  kufundishwa kwa muda mfupi na kaimu kocha mkuu wa Yanga ,Charles Mkwasa, tayari kiungo huyo ameanza  kuyakubali  maufundi anayopewa na kocha huyo.

 

Mkwasa tangu akaimu nafasi ya ukocha kutoka kwa Mwinyi Zahera aliyefukuzwa hivi karibuni, tayari kocha huyo amefanikiwa kuiongoza timu hiyo katika mchezo mmoja tu wa ligi dhidi ya Ndanda FC, ambapo walifanikwa kupata ushindi wa bao 1-0.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Balama alisema kuwa kocha huyo amewapa wachezaji morali mpya ya kupambana huku akiwapa mbinu za kukabiliana na wapinzani na muda mchache tu wamemuelewa.

“Mkwasa ni kocha mzuri, baada ya kukabidhiwa timu tu ameanza kwa kuhakikisha kuwa tunakuwa na vitu vipya, hakika huyu anaweza kutufikisha mbali.

 

“Ameanza kutupa nguvu ya kujiamini na naamini kuwa tukikaa naye muda kila mchezo tunaweza kupata ushindi na kumaliza ligi kwenye nafasi nzuri,” alisema.

Stori: Marco Mzumbe, Dar es Salaam

KAULI ya KOCHA NDAIRAGIJE Kuelekea MECHI na GUINEA “TUNAWAUA”

The post Balama Apagawa Na Mkwasa Yanga SC appeared first on Global Publishers.