NEWS

25 Novemba 2019

Eliud Kipchoge na Dalilah Muhammad waibuka washindi wa tuzo kubwa Duniani


Bingwa wa marathoni Eliud Kipchoge ameibuka mshindi wa tuzo ya mkimbiaji bora wa mwaka katika kitengo cha wanaume.

Kipchoge alitangazwa mshindi katika sherehe iliyoandaliwa na Shirikisho la Raidha Duniani (IAAF) huko Monako Jumamosi, Novemba 23 usiku. Kipchoge aliwashinda wagombea wengine wanne katika kutangazwa mshindi kwenye hafla hiyo iliyofana.

Kipchoge aliteuliwa kuwania tuzo hiyo pamoja na bingwa wa mbio za mita 10, 000 kutoka Uganda Joshua Cheptegei bingwa wa mita 200 Noah Lyles kutoka Marekani, bingwa wa mita 400 Karsten Warhorm kutoka Norwei na bingwa wa viunzi Sam Kendricks kutoka Marekani.

Kwa kitengo cha kina dada mshindi wa tuzo ya mkimbiaji bora ni Dalilah Muhammad kutoka Marekani anayekimbia mita 4000, aliwashinda Mkenya Brigid Kosgei, Mjamaika Shelly Ann Fraser na Sifa Hassan wa Uholanzi.