Msanii wa muziki na uigizaji Bongo, Hemedy Suleiman 'PHD', kupitia mahojiano aliyofanya na EATV & EA Radio Digital, amesema amesitisha kutoa mbegu za uzazi kwa wanawake ambao wanataka kupata watoto wazuri kama yeye.
Hemedy Phd amesema, sababu za kusitisha kugawa mbegu hizo za uzazi ni kuwa na watoto wengi ambao wanahitaji malezi.
"Niliamua tu kusitisha sababu nina watoto wa kutosha, sasa hivi kwanza nahitaji kuwalea kwa hiyo hayo mambo mengine baadae baadae, nina mwanamke wangu halafu tunapendana sana yaani kwa kifupi nimehangaika sana naangalia zaidi maisha natengeneza pesa" amesema Hemedy Phd.
Aidha Hemedy Phd ameendeleza kusema, sasa hivi hana mademu wengi japokuwa huwa wanamfata wenyewe.
Ikumbukwe tu kipindi cha nyuma Hemedy Phd, aliwahi kutangaza kuwa anagawa mbegu zake za uzazi bure kwa wanawake ambao wanataka kuwa na watoto wazuri kama alivyo yeye.