NEWS

20 Novemba 2019

Jaden amenitamanisha mtoto mwingine


ULISHAWAHI kusikia mtu anaambiwa ni ‘sitaki nataka’. Basi ni kama muigizaji Chuchu Hans ambaye ni mzazi mwenzake na muigizaji maarufu wa kiume Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye kipindi cha nyuma kidogo alisema hataki kuzaa tena baada ya kujifungua mtoto wake wa tatu Jayden aliyezaa na Ray, lakini sasa hivi anasema anatamani kuzaa tena.

Akizungumza na Za Motomoto News, Chuchu alisema mtoto wake Jayden anamfanya atamani kuzaa tena kwani ana uelewa mkubwa na anapendwa na kila mtu licha ya kuwa alisema hana mpango wa kuzaa tena na Ray.

“Najua kabisa zamani nilishasema sitaki kuzaa tena na Ray kwa sababu ya mambo ya hapa na pale lakini ukweli ni kwamba sasa hivi natamani na Jayden ndiye kanifanya nitamani, inabidi nikae kikao na baba yake,” alisema Chuchu.