Kupitia EATV & EA Radio Digital imempata mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Martin Kadinda, ambaye amesema huenda starehe yake ikawa ni watu kumuuliza mara kwa mara kuhusu suala la kuficha mahusiano yake.
Martin Kadinda amejibu hivyo mara baada ya kuulizwa kuhusu kuwapa mshangao watu kwanini anaficha mahusiano yake ambapo amesema,
"Nadhani ni mahusiano yangu siyo ya jamii, kila mtu anamuua jinsi gani anavyotaka kuendesha maisha yake, Mimi nimeamua kuwa nje ya vyombo vya habari kuhusu suala la mahusiano, wanaouliza waache waulize huenda ndiyo ikawa starehe yangu kuona naulizwa mara kwa mara hilo swali" ameeleza.
"Unajua mimi ni baba wa mtoto, unategemea kuna mwanaume ambaye anaweza akaishi bila mpenzi, labda ni mapadri ila siamini wanapeleka wapi vile vitu vinavyosumbua mwilini" ameongeza.