NEWS

21 Novemba 2019

Jirani Athibitisha Kusah Kumshambulia Ruby Hadi Chumba Kutapakaa Damu "Kipigo Alikipata"

Jirani athibitisha Kusah kumshambulia Ruby hadi chumba kutapakaa damu, watupiwa vyombo nje baada ya Kusah kushindwa kulipa kodi !

“Ruby na Kusah wamekuwa ni watu wa kugombana kila kukicha kiasi ambacho watu walikuwa wakigombelezea, maana huyo mwanaume alikuwa akitoa kipigo kikali bila kujua kuwa wana mtoto mmoja,” jirani huyo ameliambia Ijumaa Wikienda -

Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa, siku ya tukio, Ruby alikuwa amelala ambapo Kusah aliingia na kuchukua simu ya msanii huyo ndipo akakutana na meseji ya msanii Jux. “Alichokifanya ni kumpiga ngumi ya shingo, kisha kumshushia kipigo kikali kilichomfanya Rubby akimbilie kwa rafiki yake akiwa pekupeku huku chumba chote kikitapakaa damu.

“Kama ni kipigo tu, basi Ruby amekipata. Lakini hiki cha hivi karibuni kilikuwa ni hatari, kibaya zaidi, wakati wanagombana walikuwa wanadaiwa kodi ya shilingi laki saba, hivyo baba mwenye nyumba akawatupia virago vyao nje,” kilisema chanzo hicho

Ruby alipotafutwa na Ijumaa wikienda amesema

“Nimejiuliza maswali mengi sana kwa nini nikubali kipigo na mimi bado ni mdogo? Nimeamua kuachana naye na simtaki kabisa. Ni kweli hivyo vitu vilitolewa nje kwa sababu yeye ndiye aliyesababisha yote hayo, kwani ndiye aliyetakiwa kulipa, matokeo yake nimeambulia aibu na fedheha,” alisema Ruby huku akiomba wanasheria kuingilia kati kusaidia wanawake wanaopigwa na kunyanyaswa na wanaume. -

Kwa mujibu wa Ruby, aliamua kumsaidia baba mtoto wake huyo hasa kwenye eneo la kutoboa kimuziki kwa kumuunganisha na mastaa wakubwa kama Diamond na Jux, lakini mwisho wa siku jamaa huyo aliishia kumtusi na kumwambia kuwa anatembea nao, jambo ambalo siyo kweli kwani lengo lake lilikuwa kumsaidia mzazi mwenzie huyo nae afanikiwe Kwenye muziki