NEWS

22 Novemba 2019

Kauli ya RC baada ya Mama kumchinja na kumla mtoto


Mwanamke mmoja anaejulikana kwa jina la Christina Mlelwa(38) pichani, mkazi wa Kijiji cha Mavanga kata ya Mavanga kitongoji Cha mji mwema wilayani Ludewa mkoa wa Njombe anashikilikiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumchinja mwanae Joseph Gumbilo (4) mwenye ulemavu wa viungo na kumla.


Mwanamke mmoja anaejulikana kwa jina la Christina Mlelwa(38) pichani, mkazi wa Kijiji cha Mavanga kata ya Mavanga kitongoji Cha mji mwema wilayani Ludewa mkoa wa Njombe anashikilikiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumchinja mwanae Joseph Gumbilo (4) mwenye ulemavu wa viungo na kumla nyama.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrew Tsere, anasema mapema baada ya kufikishiwa taarifa za tukio hilo alilazimika kufika eneo la tukio na kumhoji mtuhumiwa ambaye alikiri kutekeleza mauaji ya mwanae na kisha kumkata viungo vyake.

Tukio hilo linaleta mshituko kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na kumsukuma Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka kufika katika Kijiji hicho kuzungumza na wananchi na kisha kutoa agizo kwa wakuu wote wa wilaya kukamata kijiji kizima na kuweka rumande, endapo watagoma kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu matukio ya mauaji.

Aidha Ole Sendeka ameliagiza Jeshi la Polisi kusaka ukweli wa tukio hilo haraka, na wahusika kufikishwa mahakamani kama ambavyo katiba inalinda haki ya kuishi ya kila binadamu bila kujali ulemavu wake.

Katika mahojiano ya awali Jeshi la Polisi lilieleza kuwa mama huyo ambaye anaonekana kuwa na matatizo ya akili anakiri kuuWa na kukata vipande vipande na kumla nyama.