WEMA Sepetu amesema hakuna kitu kilichomuuma na kumkosesha usingizi kama kufungwa kwa Pub ya rafiki yake, Aunt Ezekiel. Akizungumza na Amani, Wema alisema kuwa tukio hilo linamuuma sana kwa sababu rafiki huyo alijichanga muda mrefu hadi kuanzisha biashara hiyo lakini serikali imemfungia ghafla.
“Huwezi amini, ishu ya Aunt imeniumiza sana unajua kuna wakati nakosa mpaka usingizi kwa sababu najua jinsi alivyohangaika mpaka kufanikisha ile The Luxe, sasa wamemfungia unategemea nini? Lakini naamini Mungu atamuangalia kwa jicho lingine,” alisema Wema. Pub ya Aunt ilipigwa ‘bani’ na Serikali hivi karibuni kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana na kupiga kelele katika eneo hilo la Mikocheni jijini Dar.
Stori: Imelda Mtema
The post PUB YA AUNT YAMLIZA WEMA! appeared first on Global Publishers.