“KWELI jamaa amepatikana, mwanamke gani huyo anatembea naye? Halafu nasikia ana mpango wa kumuoa, yule si mwanamke hata kidogo. Ni muhuni na hafai kabisa… uliza huu mtaa mzima wakuambie, labda siku hizi kidogo ndiyo ametulia, lakini daaah! Ni moto wa kuotea mbali,” kauli kama hii ni ya kawaida sana kwenye mazungumzo ya watu huko mitaani. Utakuta mtu anazungumzwa kwa mabaya aliyowahi kufanya huko nyuma, anahukumiwa na wakati mwingine hata mwenzi wake anapewa taarifa hizo.
Hapo ndipo panapoibua matatizo. Marafi ki zangu, lengo la mada hii ni kuangalia kama tabia au mwenendo wa zamani wa mtu unaweza kuathiri uhusiano mpya hasa kama amebadilika tabia. Je, tabia zake za huko nyuma zinapaswa kutumika kama kigezo cha kupima penzi la dhati? Ni mada inayohitaji utulivu wa akili sana, hebu kwanza twende tukaone kipengele kinachofuata.
SIKILIZA USHUHUDA HUU;
Baada ya mada hii kutoka katika sehemu ya kwanza wiki iliyopita, nilipokea simu na meseji nyingi sana. Wapo waliokiri juu ya tabia zao za nyuma. Tumsikie mmoja wao. Huyu hapa; “Nakubali huko nyuma nilikuwa na tabia mbaya sana, nilikuwa nalewa na nikienda club naweza kurudi alfajiri au nikalala hukohuko. Nimetembea na wanaume wengi sana, lakini sasa nimekuwa na nimeachana na tabia za kijinga. “Kilichonifanya nikutumie huu ujumbe ni kwamba, mpenzi wangu alivyoanza kunichunguza akaambiwa mambo lukuki ya nyuma. Alivyoniuliza, nilikiri.
Nilimweleza ukweli wa kila kitu, lakini nilimhakikishia kwamba nimeamua kwa dhati kubadilika na asitarajie kuwa nitaendelea na tabia za zamani. Nashukuru mpenzi wangu ni muelewa na mipango yetu ya ndoa inaendelea kama kawaida.” Marafi ki zangu, bila shaka kuna kitu mmejifunza hapo.
Wakati mwingine kuwa mkweli kwa mwenzako na kumweleza hali halisi kunaweza kumfanya azidi kukuamini na kuendelea kukupa nafasi kubwa katika maisha yenu. “KWELI jamaa amepatikana, mwanamke gani huyo anatembea naye? Halafu nasikia ana mpango wa kumuoa, yule si mwanamke hata kidogo.
Ni muhuni na hafai kabisa… uliza huu mtaa mzima wakuambie, labda siku hizi kidogo ndiyo ametulia, lakini daaah! Ni moto wa kuotea mbali,” kauli kama hii ni ya kawaida sana kwenye mazungumzo ya watu huko mitaani. Utakuta mtu anazungumzwa kwa mabaya aliyowahi kufanya huko nyuma, anahukumiwa na wakati mwingine hata mwenzi wake anapewa taarifa hizo. Hapo ndipo panapoibua matatizo.
Marafi ki zangu, lengo la mada hii ni kuangalia kama tabia au mwenendo wa zamani wa mtu unaweza kuathiri uhusiano mpya hasa kama amebadilika tabia. Je, tabia zake za huko nyuma zinapaswa kutumika kama kigezo cha kupima penzi la dhati? Ni mada inayohitaji utulivu wa akili sana, hebu kwanza twende tukaone kipengele kinachofuata.
SIKILIZA USHUHUDA HUU;
Baada ya mada hii kutoka katika sehemu ya kwanza wiki iliyopita, nilipokea simu na meseji nyingi sana. Wapo waliokiri juu ya tabia zao za nyuma.
Tumsikie mmoja wao. Huyu hapa; “Nakubali huko nyuma nilikuwa na tabia mbaya sana, nilikuwa nalewa na nikienda club naweza kurudi alfajiri au nikalala hukohuko. Nimetembea na wanaume wengi sana, lakini sasa nimekuwa na nimeachana na tabia za kijinga. “Kilichonifanya nikutumie huu ujumbe ni kwamba, mpenzi wangu alivyoanza kunichunguza akaambiwa mambo lukuki ya nyuma.
Alivyoniuliza, nilikiri. Nilimweleza ukweli wa kila kitu, lakini nilimhakikishia kwamba nimeamua kwa dhati kubadilika na asitarajie kuwa nitaendelea na tabia za zamani. Nashukuru mpenzi wangu ni muelewa na mipango yetu ya ndoa inaendelea kama kawaida.” Marafi ki zangu, bila shaka kuna kitu mmejifunza hapo.
Wakati mwingine kuwa mkweli kwa mwenzako na kumweleza hali halisi kunaweza kumfanya azidi kukuamini na kuendelea kukupa nafasi kubwa katika maisha yenu. MSOME Kwa sababu umepewa taarifa hizo na watu, kazi yako kubwa sasa inatakiwa kuwa ni kumsoma kama kweli mwenzi ana hizo tabia.
Kwa sababu unamfahamu vizuri inaweza kuwa rahisi zaidi kupata majibu sahihi katika uchunguzi wako. Linganisha ulichoelezwa au gundua tabia zake za sasa. Je, ni kweli hajaacha? Unaweza kwenda mbele zaidi hata kwa kumpima na kumuwekea mitego. Kama ni tabia yake atanasa tu. Kuujua ukweli itakuwa hatua ya kwanza wakati ukifi kiria hatua ya pili ya nini cha kufanya.
MPE MIFANO
Inawezekana umemchunguza vya kutosha na umegundua kwamba mwenzako hana tabia hizo au kama alikuwa nazo ni huko nyuma na sasa amebadilika. Wengi hawapendi kujulikana siri zao za nyuma. Lakini ili uwe huru zaidi kwenye uhusiano wenu na mapenzi yaongezeke ni vyema kama mwenzako atakiri mbele yako juu ya tabia zake za awali hasa kwa sababu tayari umeshagundua. Hili ni jambo gumu kwa sababu hafahamu kama umegundua, pia ana wasiwasi kuwa
ukigundua unaweza kumuacha. Zungumza naye kwa akili, mpe mifano. Msogeze kwenye ukweli; mwambie jinsi ambavyo huna moyo wa kuhukumu kwa makosa yaliyopita. Mweleze unavyopenda mtu anayesema ukweli kuliko kugundua mwenyewe. Hii itamsaidia kuwa huru na pengine anaweza kukueleza ukweli. Hapa sasa itakuwa nafasi yenu kuzungumza kwa upendo na kuweka mikakati ya kudumisha uaminifu katika penzi lenu. JE, UNAMPENDA? Je, unampenda?
Anakupenda? Kama ndivyo, ya nini kujiumiza kichwa kwa mambo yaliyopita badala ya kujenga uhusiano imara na wenye nguvu? Uamuzi upo mikononi mwako. Mada imeisha. Hadi wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri, USIKOSE! Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vya True Love, Let’s Talk About Love na All About Love. Kwa sasa anaandaa kitabu chake kipya cha SIRI ZA NDOA YENYE FURAHA kitakachoingia mitaani hivi karibuni
The post UKIANGALIA MBELE UTAYAFURAHIA MAISHA YA UHUSIANO!-2 appeared first on Global Publishers.