NEWS

30 Desemba 2019

Jeshi La Polisi Mkoani Mbeya Lakamata Watuhumiwa 12 Wa Makosa Mbalimbali Ya Uhalifu Ikiwemo Na Kukutwa Na Sare Za Jeshi La JWTZ

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa kumi na mbili [12] kutokana na tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya [bhangi], pombe haramu ya moshi [gongo], mali za wizi na pombe kali zilizopigwa marufuku nchini. Watuhumiwa wamekamatwa katika misako na doria zinazoendelea hapa Mkoani Mbeya katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka.

KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 27.12.2019 majira ya saa 15:00 Alasiri huko Kijiji cha Shigamba, Kata ya Utengule - Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya.  Askari Polisi waliwakamata 1. SAKA JAKOBO [20] 2. GODIUSI NAZARETY [23] 3. ERASTO YOHANA MWAMPAMBA [25] na  4. DENISI EDWARD [22] wote wakazi wa Shigamba wakiwa na bhangi gramu 35. Watuhumiwa ni watumiaji na wauzaji wa bhangi.

KUPATIKANA SARE ZA JESHI LA WANANCHI TANZANIA [JWTZ].
Mnamo tarehe 27.12.2019 majira ya saa 15:00 Alasiri huko Kijiji cha Shigamba, Kata ya Utengule - Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata ISAKA JAKOBO [20] mkazi wa shigamba akiwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania [JWTZ] ambazo ni mkanda mmoja, kofia moja rangi ya kijani “crown” mbili, begi moja la mgongoni, kofia moja rangi nyekundu, nishani mbili na mkanda mmoja wa “RSM”. Mtuhumiwa pia alikutwa akiwa na pikipiki Na. MC 852 BLE “Boxer” rangi nyeusi inayodhamiwa kuwa ni mali ya wizi.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Mnamo tarehe 28.12.2019 majira ya saa 16:00 jioni huko Mapeleme, Kata ya Ubaruku, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata ESTWITA KILIMA [42] mkazi wa Mapelema akiwa na pombe haramu ya moshi[gongo] lita 28. Mtuhumiwa ni muuzaj na mtumiaji pombe hiyo.

KUPATIKANA BHANGI.
Mnamo tarehe 29.12.2019 majira ya saa 13:00 mchana huko maeneo ya Kibisi, Kata ya Kyimo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata AMBOKILE MWAISABILA [38] mkazi wa Kibisi akiwa na bangi kilogram 12. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi.

KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.
Mnamo tarehe 29.12.2019 majira ya saa 18:00 jioni huko mtaa wa DDC – Mbalizi, Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata GADI CHARLES [19] mkazi wa DDC akiwa na miche 7 ya bhangi ndani ya shamba lake la mahindi. Mtuhumiwa ni mtumiaji wa bhangi.

KUPATIKANA NA POMBE ZILIZOKATAZWA NCHINI.
Mnamo tarehe 29.12.2019 majira ya saa 16:30 jioni huko Kijiji cha Talatala, Kata ya Ipinda, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata ROSTA MWASAMBOGO [31] mkazi wa Talatala akiwa na “Win” boksi mbili na boksi moja “Cafe rhum” kutoka nchi ya Malawi.

KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO YA WIZI.
Mnamo tarehe 29.12.2019 majira ya saa 16:00 jioni huko mtaa wa Mapelele - Mbalizi, Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa Mbeya. Askari Polisi walimkamata EZEKIA MIKISON [40] mkazi wa Mapelele akiwa na TV “Sundar” inch 19 inayodhamiwa kuwa ni mali ya wizi.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Mnamo tarehe 29.12.2019 majira ya saa 14:45 mchana huko Kitongoji cha Itete - Ndembo, Kata ya Kabula, Tarafa ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata TUNU KIJUMILE [21] mkazi wa Ndembo akiwa na Pombe haramu ya Moshi [gongo] lita 3. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Mnamo tarehe 29.12.2019 majira ya saa 18:00 jioni huko Kitongoji cha Majengo - Mapya, Kijiji na Kata ya Lupa, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata ANNA WESTON [40] mkazi wa Lupa akiwa napombe haramu ya moshi [gongo] lita sita ndani ya nyumba yake. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Mnamo tarehe 28.12.2019 majira ya saa 16:00 jioni huko maeneo Igogwe, Kata ya Kawetele, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata SAMSOM MWAKYUSA [23] mkazi wa mtaa wa Bagamoyo akiwa na pombe haramu ya moshi [gongo] lita 17. Mtuhumiwa ni muuzaj na mtumiaji pombe hiyo.

Imetolewa na;
[ULRICH O. MATEI – SACP]
   KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.