Shirika la afya ulimwenguni, WHO kwa mara nyingine linataraji kuitisha kikao cha kamati yake ya wataalamu baadae hii leo ili kujadiliana kuhusu iwapo wanaweza kutangaza mripuko wa virusi vya Corona kama dharura ya afya duniani.
Virusi hivyo tayari vimeshawaua watu zaidi ya 160 na zaidi ya watu 7, 711 wameambukizwa tangu kulipotambuliwa mgonjwa wa kwanza katika jiji la Wuhan nchini China, Disemba 31.
Mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Gebreyesus, aliyerejea kutoka China amesema ilikuwa ni muhimu kuitisha mkutano mwingine, ambao ni wa tatu kwa wiki hii kwa kuwa virusi hivyo vimekwishasambaa hadi nje ya China, akisema ni hali inayozidi kutia wasiwasi.
Nchi wanachama wa timu hiyo ya WHO iliamua wiki iliyopita kwamba janga hilo lilikuwa bado halijafikia kiwango cha kutangazwa dharura ya dunia.
Hatua kama hiyo ilitangazwa na WHO wakati wa mripuko wa Ebola na mafua ya ndege