NEWS

4 Septemba 2020

Ditopile: Magufuli kaunganisha kila Mkoa na Barabara ya lami


Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma (CCM), Mariam Ditopile ameshiriki kampeni za uzinduzi wa Chama hicho Jimbo la Kibakwe wilayani Mpwapwa na kumuombea kura Mgombea Urais wa chama chake, Dk John Magufuli, mgombea ubunge, George Simbachawene na madiwani 18.

Akizungumza katika kampeni hizo, Ditopile amewasihi wananchi wa Kibakwe kutokufanya makosa kwa kuwachagua wapinzani ambao kazi yao imekua kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali badala ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Ditopile amesema ndani ya miaka mitano ya kwanza ya Magufuli Mkoa wa Dodoma umenufaika na miradi mingi mikubwa ikiwemo vituo vya afya ambavyo Jimbo la Kibakwe lilinufaika navyo, elimu bure na upatikanaji wa nishati ya umeme wa vijijini REA.

 " Ndugu zangu wa Kibakwe niwasihi mchague CCM, hawa wapinzani hata wagombea hawana wanasubiri wanaotoka kwetu ndio wawachukue, hivyo siyo vyama vya kuwapa Nchi, sasa kama hawana wagombea wa kuwasimamisha ndio sisi tuwaamini kweli? Niwasihi Oktoba 28 msifanye makosa nendeni mkaichague CCM kwa ajili ya kuwaletea maendeleo.

" Wote ni mashahidi Magufuli ameziishi ahadi zake, alisema anataka kuwatetea wanyonge na ndio sababu miaka mitano yote kamaliza bila kwenda nje ya Nchi licha ya kwamba amenunua Ndege 11, kila siku utamsikia Kigoma, Singida kote huko kwa ajili ya kuwasikiliza na kuwatumikia watanzania ambao walimchagua," Ditopile.

Amesema kwa mambo makubwa yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Dk Magufuli kwa miaka mitano iliyopita ni wazi anastahili m