NEWS

29 Septemba 2020

Google yazifutilia mbali App 17 kisa uharifu wa taarifa kwa watumiaji wake



Mtandao wa CNN, umeripoti kuwa Wataalamu wa kampuni ya Google wamezifutilia mbali App 17 za Android kwa kukutwa na makosa ya kuiba taarifa za watumiaji wake.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kubaini wizi huo wa taarifa ulifanywa kwenye jumbe za simu, orodha ya kwenye mawasiliano na taarifa za kifaa husika (device) pia kwa kujisajili kwenye WAP (wireless application protocol) bila ridhaa ya mtumaji.


Watumiaji wa App hizo wanashauriwa kuziondoa haraka (uninstall) kwenye orodha ya app kwenye simu zao.


Mfumo wa  google play huwa unafanya ukaguzi kubaini kugundua programu hatari na zenye zengwe. Imeelezwa.


App hizo ni Direct messenger, All Good PDF scanner, Unique keyboard – fancy fonts & free emoticons, Mint Leaf Message – Your private message,Tangram App Lock, Private SMS, One Sentence Translator, Style Photo Collage, Desire Translate, Meticulous Scanner, Talent Photo Editor, Care Message, Part Message, Paper Doc Scanner , Blue Scanner, All Good PDF scanner, Hummingbird PDF Converter.