Polisi mkoani Manyara wameripoti kuwatia mikononi watuhumiwa 6 wa madawa ya kulevya aina ya Bangi misokoto 36 na wengine 11 wakiwa na Pombe haramu Gongo lita 139.5 na mmoja akiwa na mitambo ya kuchemsha Pombe hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Paul Kasabago amearifu kwamba operesheni ilitekelezwa kuanzia Agosti 20,2020 hadi Septemba 4,2020 kwa lengo la kuwakomboa wanannchi katika utumiaji wa madawa hayo.
Aidha Kasabago amesema katika Operesheni hiyo wamewakamata watu 9 wakiwa na mali ambazo zinadhaniwa kuwa ni za wizi ambazo ni Cherehani moja aina ya Butterfly, Jiko la gesi moja aina ya Opex ambazo zote zina thamani ya shilingi 195,000 pamoja na Generator aina ya Honda H2000 na Speaker moja zenye thamani ya shilingi 2,500,000 moja ambazo ni mali ya Kanisa la Tanzania Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo wilaya ya Hanang’.
Amesema katika operesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 25 walikamatwa na wote wamefikiswa mahakamani kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili na kesi zao zipo katika hatua za kutajwa na zingine kusikilizwa.
Kamada Kasabago amewataka wale wanaofanya biashara haramu kuacha mara moja na kutafuta biashara zingine zitakazoweza kuwaingizia kipato kwa njia halali.