NEWS

4 Septemba 2020

TAWA Yakabidhi Jengo Ofisi Ya Mkurugenzi Mkuu Wa Mashitakanchini (DPP) Kahama

SALVATORY NTANDU
Mamlaka ya Wanyamapori   Tanzania (TAWA) imeikabidhi ofisi ya taifa ya Mashitaka chini ya DPP   jengo lililokuwa likitumiwa na mamlaka hiyo kanda ya Kigosi lililopo wilayani kahama mkoani  Shinyanga baada ya mapori waliyokuwa wakiyasimamia kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi  za taifa ambapo jengo hilo litatumika kuendesha kesi za jinai ikiwa ni mkakakti wa serikali wa kupunguza Msongamano wa  maabusu na waafungwa  katika  Magereza nchini

Akizugumza Jana baada ya Makabidhiano ya jengo hilo Kaimu Kamishina wa uhifadhi nchini Mabula  Nyanda amesema kuwa kutokana na uhusiano  uliopo kati ya  ofisi yake na ofisi DPP  wamekuwa wakishirikiana katika masuala ya uendeshaji wa kesi za makosa  yaliyokuwa yakihusika na rasimali za wanyama pori ambapo   wameamua kuwapatia  jengo  hilo kwa muda ili waweze kusaidia jamii katika kesi mbalimbali

“Kama mnavyojua moja ya kazi muhimu sana katika taasisi hizi ni ulinzi wa rasimali za wanayamapori ambazo ni kazi za hima sheria kama mnavyojua ziko nne kwanza kuna operation, ukusanyaji wa taarifa, uendeshaji wa mashitaka na upelelezi hizi zote ni zinahusika na mashitaka,”amesema  Kaimu Kamishina Nyanda

Amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana sana na ofisi ya taifa ya mashitaka katika kesi zote ikiwemo zinazohusu usimamizi wa rasilimali za wanyamapori ambapo DPP amekuwa msaada mkubwa wa kupambana na uharifu kwenye  ujangili,mifugo na uvamizi wa mapori ya akiba hivyo tumeona umuhimu wa kuwapa jingo hili.

“Sisi tulikuwa tunatumia ofisi hii ya Kanda ya kigosi toka hapa Kahama baadae serikali ikapandisha hadhi mapori hayo toka pori la akiba hadi  kuwa hifadhi, hivyo tukaaamua kupisha na tulikuwa na mpango wa kuwekeza  mradi, ndipo tukapokea maombi toka kwa mdau wetu muhimu ofisi ya DPP wakitaka tuwapatie kwa ajili ya kufungua ofisi ya taifa ya  mashitaka ya wilaya ya kahama  nasi hatukuwa na shida tukaamua kumpa kwa muda kwa ajili ya utekeleza wa kazi zake za kuhudumia wananchi”

Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka nchini Bishwalo Mganga  amesema  kuwa kutokana na idadi kubwa ya  watu walikuwa wakisafiri kwenda kupata huduma mkoani Shinyanga  hali amabyo ilikuwa inachangia kuchelewa kutolewa kwa maamuzi hivyo kusogezwa kwa huduma hiyo wilayani kahama itasaidia kupungza adha ya kusafiri umbali mrefu.

“Tumeamua kufungua ofisi hapa kwa sababu gereza la kahama linapokea watu wengi kwa sababu linapokea kutoka wilaya jirani za Mbogwe na Bukombe zilizoko Mkoani  Geita  hivyo kuna kesi amabazo hazina ulazima sana wakili wa serikali atazichuja na kuzitoleea maamuzi nay ale yanayoshindikana yanakuja kwetu”

Biswalo amesema kuwa uwepo wa ofisi hiyo wilayani kahama utasaidia kupunguza  Msonagamano  ulioko kwenye gereza hilo pamoja na kuhakikisha kwamba kesi zinaendeshwa mapema na kwa mujibu wa sheria huku ofisi yake ikiendelea na mkakati wa kuwa na majengo ya ofisi zake

Naibu Katibu Mkuu wizara ya katiba na sheria Amon Mpanju amesema kuwa nchi haiwezi kuwa na amani pasipo uwepo wa ofisi ya Taifa ya mashitaka  hivyo  uwepo wake ni muhimu sana katika kuhakikisha amani inadumu  huku akibainisha kuwa mara baada ya kutembelea gereza la kahama  ni jambo jema lililofanywa na DPP la kuomba kupewa jingo kwa ajili ya kuanzisha ofisi hiyo.

“Ni vema ushirikiano huu ukaendelezwa kati  ya TAWA na DPP ili kuhakikisha  Ulinzi wa Rasilimali za nchi zinaendelea kulindwa na kutunzwa kwa mujibu wa sheria za nchi nimefurahi sana kwa hili lililofanyika leo kuamua kuwapa jengo hili ofisi ya DPP nanyi hakikisheni mnalitunza ili hata mkiondoka libaki katika ubora  wake”

Naye katibu tawala wa wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya  amesema kuwa kwa sasa wilaya hiyo ina idadi  kubwa ya wakazi takribani milioi moja hali inayochangia kuongeza vitendo vya uharifu na ongezeko la makosa ya jinai hivyo uwepo wa Ofisi ya DPP  utasiadia kuondoa kero  kwa wananchi ikiwemo ucheleweshwaji wa kesi.

Mkuu wa Magereza Mkoani Shinyanga, Kamishina Msaidizi Elizabeth Mbezi amesema iwapo itaanza kufanya kazi ofisi ya mshitaka ya taifa itasiadia kupunguza kesi za watuhumiwa ambao hawana ulazima sana wa kukaa gerezani pamoja kupunguza Msongamano wa Mahabusu ndni ya gereza

“Kwa sababu  Gereza letu la Kahama linapokea watuhumiwa toka halmashauri tatu wa wilaya hii pamoja na wilaya jirani za Mbogwe na Bukombe ambao hutumia gereza hilo kwa hiyo ifsis hii itasiadia kurahisisha mahabusu ambao si lazima kwenda gerezani kesi zao zikaishia nje”amesema Mbezi

Mwisho