Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imemteua Maalim Seif Sharif Hamad kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika 27 na 28 Oktoba 2020.
Maalim Seif alikuwa miongoni mwa wagombea 17 waliokuwa wamechukua fomu kuwania urais wa Zanzibar lakini jana Alhamisi tarehe 10 Septemba 2020 ilifanya uteuzi wa wagommbea 16 na Maalim Seif akiwekewa mapingamizi.
Mapingamizi hayo yaliwekwa na vyama vya DP na Demokrasia Makini wakidai fomu za Maalim Seif aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar zina kasoro