NEWS

2 Oktoba 2020

Uganda imetangaza kuwa itawatoa hospitali wagonjwa wa Covid-19 bila kupimwa



Wizara ya Afya ya Uganda imefanyia marekebisho muongozo wake wa kukabiliana na corona ambayo itawafanya wagonjwa wa Covid-19 wasioonesha dalili ya maambukizi kutolewa hospitali bila kufanyiwa tena uchunguzi.

Wiziri wa Afya Jane Ruth Aceng amesema watu waliotengwa kwa siku 10 watatolewa hospitali ikiwa hawataonesha dalili ya maambukizi.

”Hii itapunguza msongamano wa wagonjwa wanaosubiriwa kufanyiwa uchunguzi tena kabla ya kutolewa hospitali”, alisema B Aceng.

Awali wagonjwa walikuwa hawawezi kutolewa hospitali hadi wapimwe mara ya pili kuhakikisha hawana virusi vya corona. Lakini baadhi ya owalilalamikia muda wanaosubiri kufanyiwa vipimo hivyo vya lazima licha ya kuwa hawaoneshi dalili ya kuwa wagonjwa.