NEWS

6 Julai 2022

Balozi Za Tanzania Kuadhimisha Siku Ya Kiswahili


Na Shamimu Nyaki – WUSM

Serikali imeelekeza Balozi zote za Tanzania Ulimwenguni kuhakikisha inaadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani Julai 07, 2022.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Saidi Yakubu wakati  akitoa neno la Utangulizi  katika Maadhimisho ya Kiswahili Duniani ambapo l Julai 05, 2022 ni Kiswahili na Elimu, Wachapishaji, Wasanii na Wanafunzi  ambayo inaongozwa na Mdahalo maalumu kuhusu lugha yetu.

Tumeelekeza Balozi zetu kote Ulimwenguni kuhakikisha tarehe 07, 2022 wanaadhimisha Siku ya Kiswahili, siku hiyo tunataka Dunia itambue lugha hiyo kuwa  Chimbuko lake ni Tanzania. Tunaamini Balozi hizo zitasaidia Kutangaza vyema lugha hiyo na kutoa fursa kwa watanzania katika kupata ajira ya kufundisha lugha hiyo Duniani” amesema Saidi Yakubu.

Ameongeza kuwa, Tanzania pia itashiriki katika maadhimisho hayo nchini Ufaransa katika Makao Makuu ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambapo itawakilishwa na baadhi ya Mawaziri  pamoja na Msanii Mrisho Mpoto.

Bw. Yakubu amesema kuwa, katika Kilele Cha Siku ya Kiswahili Duniani Julai 07, 2022 Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere JNICC, Dar es Salaam.