Mara baada ya mchezo huo kuna video iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha Afisa huyo wa Yanga akijibizana au kutupiana maneno na Rais wa TFF Wallace Karia huku wengi wakitafsiri kuwa Manara alikuwa akimtukana Rais huyo.
Akiongea na waandishi wa habari Manara amesema kuwa alikosea kujibizana na Rais hadharani huku akiweka wazi kuwa yupo tayari kuwajibishwa iwapo itaonekana. Inastahili.
''Nilienda kumuona rais wa TFF nyumbani kwake, kumuomba radhi juu ya kilichotokea naamini mimi nikama mwanae natumaini atakuwa amenielewa"amesema Haji Manara.