NEWS

6 Julai 2022

Bweni La Wavulana Chalinze Modern Islamic Lateketea Kwa Moto


Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
BWENI la Wavulana Chalinze Modern Islamic Primary School , Mkoani Pwani limeungua  Moto ,alfajiri ya Julai 5 mwaka huu ,ambapo mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alfika Shuleni hapo kujionea hali halisi ya janga hilo.
 
Katika janga Hilo la Moto hakuna vifo, madhara yeyote makubwa yaliyojitokeza .
“Nichukue nafasi hii kuutarifu umma  tumepata Changamoto ya tukio la Moto katika Shule yetu hii ya Chalinze Islamic Modern school  ,tunamshukuru Mwenyezi Mungu hatukupata Madhara yanayohusisha athari za kifya na maisha ya wototo wetu,wakiwa katika nyumba ya ibada msikitini “Ameeleza Kunenge.
 
Ameeleza ,Vitu ikiwemo Sare, mabegi, sabuni, na baadhi ya madaftari walivyokuwa wakikaa navyo kwenye Bweni ndivyo vimeteketea kwa moto. 
Ameeleza Shule hiyo ni kubwa wanafunzi ambao bweni lao limeungua wamepata mahali pengine pa kulala. 
 
Hata hivyo ,Ameeleza Wataalamu tayari wameongea na vijana hao kuwatoa hofu na kuwashauri.
Kunenge amelishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani hapo kwa Elimu wanayotoa kwa Shule za Mkoa huo katika Uthibiti wa Mioto
Kunenge ametoa Rai kwa Shule zote za Mkoa huo kupata Mafunzo hayo ya Elimu jinsi ya kuthibiti madhara ya moto hatua za awali,kwenye hatua ya Ujenzi vitu gani viandaliwe,  na endapo moto unatokea nini cha kufanya.
 
“Shule hii ilipokea Mafunzo mwezi mmoja uliopita na Moto huu ulipotokea Vijana na Jumuiya ya Wafanyakazi wa shule hii wamethibiti moto huu kutumia vizimia Moto (Mitungi) kabla gari la zimamoto halijafika” Ameeleza Kunenge.
 
Ameeleza ni “Fundisho zuri kwamba  Elimu wameapata na Uongozi wa shule ulihakisha Uwepo wa vifaa vya  Vizimia moto” amewaeleza Kunenge.
 
Mkuu huyo wa mkoa, ameunda timu ya kitaalamu ya kuchunguza   chanzo cha moto huo ili kuchukua hatua zitakazosaidia  Shule hii na Shule zingine Mkoani hapo.