Ujio wa Zuriel nchini Tanzania ulikuwa sehemu ya ziara yake ya Afrika Mashariki katika uzinduzi wa program yake ya Dream Up, Speak Up, Stand Up yenye lengo la kuwahamasisha wasichana wa kiafrica.
Zuriel akiwa na mama Salma Kikwete
October 11 Zuriel alihudhuria tukio lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa UNFPA Dar es salaam ambalo lililenga kupunguza ndoa za utotoni kwa Tanzania.
Binti huyo ambaye makazi yake ni California, Marekani kwa sasa pia alialikwa Mama Salma Kikwete kumtembelea. Katika mwaliko huo Mama Salma alimsifia Zuriel kwa kuhamasisha maswala ya elimu kwa watoto wa kike kwa viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika na kumchagua kuwa balozi wa WAMA.
Ingia hapa kumfahamu zaidi Zuriel Oduwole.
Source: informationng.com Picha: Full Shangwe Blog


