
“Safari ni mwezi wa 11 sababu (Fally Ipupa) alikuwa tour kwahiyo natakiwa niende. Namshukuru Mungu kunikubalia kwake, na mimi pia nimejikusanya sababu nadunduliza, sina mtu wa kunisaidia, ningepata mtu wa kunisaidia ingekuwa ni vizuri zaidi. Lakini namshukuru Mungu najikongoja hivyo hivyo, nitafika salama kwa uwezo wa Mungu,” alisema H.Baba.