baada ya utawala wake kwa miaka yote hii ilipofika mwaka jana kuna “chalii” mmoja wa arusha alianza naye kufanya videos.jamaa anajulikana kama nisher. mshkaji alianza kufanya video fulani hivi za maunderground na kama wewe sio mfuatiliaji mzuri wa videos za bongo unaweza kufikiri kwamba video ya kwanza nsher kuifanya ikawa ni sijutii ya joh makini au listen ya belle 9 , lakini siyo kweli. nisher alikua na video zake nyingine ambazo zilikua hewani.
Baada ya nisher kukubalika sana na watu kwa kufanya video nzuri watu wengi walianza kumpa sifa za kutosha na wengine kudiriki kumvua ufalme wa video adam juma kitu ambacho kilizua utata. miezi saba iliyopita adam juma aliamua kuvunja ukimya na kutupia comments zake kwa youtube katika video ya mama yeyoo ya G.nako feat ben pol aliyoifanya nisher. adam juma alimponda nisher kwa kutumia filters na effects .