
“Mimi sijachumbiwa na hakuna mtu yeyote aliyenichumbia na kama itatokea siku nikachumbiwa kila mtu atajua, na ni mimi mwenyewe ndiye nitakaesema,” alisema mrembo huyo.
“Lakini sasa sijajua wao wamepata hiyo habari kutoka kwenye chanzo gani, by the way kwaajili kumekuwa na habari kila kukicha kila mtu anayejisikia kuandika anaandika ,anaamka anaandika, anaamka anandika. Kwahiyo leo wameandika nimechumbiwa, kesho wataandika nimeolewa, kwahiyo inategemea na mood ambayo wao waliamka nayo, kwamba ‘leo Lulu tumchumbie, tumuozeshe, tumuachishe’, I don’t know.
“Kuchumbiwa, kuolewa,kuwa mke ni vitu ambavyo tumeumbiwa binadamu, vipo kama ukiwa mpango wa mwenyezi Mungu nitachumbiwa na nitaolewa.”