Katika club hiyo ya Kidoti itakua ikijihusisha na maswala ya kutoa ushauri katika jamii ikiwa pamoja na taarifa za kimuziki, filamu na kazi za kisanaa kiujumla kwa kila rika katika jamii, Kidoti Club lengo lake kubwa haswa ni kupanua mtandao wake kwa jamii na kuwapa nafasi watu wengine waweze kujiunga.
Esther Wassira (kulia) akisoma ujumbe mara baada ya kujiunga na Club ya Jokate, katikati ni Jokate na wa kwanza kushoto ni Bhoke wa EATV
“Huu ni mfumo wa kisasa katika kutoa taarifa mbalimbali kwa jamii. Beyonce amefanya hivyo na kwa sasa hakuna mtu anayeingia katika shoo zake bila kuwa mwanachama wa klabu yake. Mimi pia naelekea huko kwani nitaweka taarifa zangu mbalimbali na ili kupata lazima uwe mwanachama,” alisema Jokate ambaye pia ni mtangazaji na mbunifu wa mavazi.
“Kama unavyojua, lengo langu kubwa ni kutumia ujuzi na kipaji changu kwa watanzania wote, nataka wafaidike na vipaji vyangu nami kusimama mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu yoyote. Natoa wito kwa vijana wenzangu kuwa wabunifu katika kukabiliana na masuala mbalimbali ya maisha.”
** Jokate alisema kuwa kupitia klabu yake atakuwa anatoa ushauri mbal mbali katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa za muziki, filamu, wasanii mbalimbali na nyinginezo kwaajili ya rika tofauti.**


