Utuaji huo ulikuwa wa hatari kwakuwa njia ya ndege ya uwanja huo ina urefu wa mita 1.620 ama futi 5.315, urefu ambao ni mdogo mno kwa ndege hiyo ya Boeing 767-383ER kutua.
Uwanja wa ndege wa Arusha hauwezi kumudu ndege yenye ukubwa kama hiyo ya Ethiopian Airline kutua
Ndege hiyo yenye namba ET-AQW ilikuwa inatokea Addis Ababa kwenda Zanzibar kupitia Kilimanjaro. Hakuna aliyeumia kwenye utuaji huo uliosababisha uwanja wa ndege wa Arusha ufungwe kwa muda.
Kuna taarifa kuwa ndege hiyo ilishindwa kutua KIA kwakuwa kulikuwa na ndege iliyokuwa imeziba njia na hivyo kuamua kwenda Arusha kwakuwa uwezakano wa kwenda kwenye uwanja wa ndege unaomudu ukubwa wake ulikuwa mkubwa kwakuwa ndege hiyo haikuwa na mafuta ya kutosha.
Picha Via :RegionalAirServices




