Tunafahamu kuna majina tayari yanayotajwa kuwa huenda wakawa ndio msichana huyo lakini hatuwezi kuyataja wala kuthibitisha kwa sasa ili kuepuka kuripoti habari zisizo na ukweli. Mtandao wa chinadaily.com.cn umeandika habari na kuweka picha za kukamatwa kwa msichana huyo mwenye umbo refu, mwenye nywele ndefu na mweupe.
Mtandao huo umeandika: Msichana mwenye miaka 28 kutoka Tanzania alikamatwa kwa tuhuma za kumiliki madawa ya kulevya huko -Macao, Dec 19, 2013. Alikuwa ameficha kilo 1.1 za heroin zenye thamani ya $137,720 ( sawa na zaidi ya shilingi milioni 85) ndani ya mwili wake na kuchukua ndege kutoka Thailand hadi Macao. Alisema alikuwa akielekea Guangzhou, mji mkuu wa jimbo la Kusini mwa China Guangdong.
Madawa yaliyotolewa kwenye mwili wa msichana huyo mwenye miaka 28 yakioneshwa mbele ya waandishi wa habari
Adhabu ya makosa ya biashara za madawa ya kulevya nchini China ni kifo.
Source;Bongo5