Msanii Huyo aliyetembelea Studio Za Magic fm Akiongozana Na mkubwa Fela Pamoja Na Babu Tale kwa nia ya Kuja kuomba Msamaha na kuweka mambo sawa alifunguka kupitia kipindi cha Daladala Beats Kinachoruka Magic Fm Kuanzia Saa saba mchana mpaka saa kumi jioni
Ni Takriban Mwaka Mmoja Na Nusu Tangu Nyimbo za Msanii Huyo Kuacha kuchezwa na kituo hicho baada ya Misunderstanding hiyo kujitokeza.
Tangu jana kupitia vipindi mbaali mbali nyimbo za Diamond Zimeanza Kuskika Tena kupitia kituo hichi baada ya kurejesha tena maelewano baina ya kituo na msanii huyo
Diamond pia alizungumzia wimbo wake mpya wa My Number One Remix Aliofanya na msanii Davido wa Nchini Naijeri, na hilo ndo Pini jipya lililopo sokoni sasa kwa msanii huyo anayetajwa kuwa mkali zaidi bongo kwa sasa
Picha Wakati Msanii Diamond Akiwa Katika Studio Za Magic Fm Kuyamaliza
Kamati hiii ndio imesaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza tofauti hizi za Diamond Na Magic Fm Radio, Kushoto Ni Meneja Msaidizi wa Magic Fm Dizzo One, Dativus Mango Radio Manager Magic Fm, Mkubwa Fela na Babu Tale Ambao ni wasimamizi wa kazi za Diamond
Diamond katika mahojiano na Dj Tass wa kipindi cha Dala dala Beats
Diamonda Ndani Ya Studio Za Magic Fm Akizugumza
Wasuluhishi, Babu Tale, Dativus Mango Radio Manager Magic Fm, Na Mkubwa Fela
Mish B sambamba na Mdogo wake Diamond na Musa Kipanya
Musa Kipanya Diamond NA Salma Msangi