Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa leo na CAF kupitia kwa naibu mkurugenzi wa mashindano Bwana KhaledNassar, Uwanja wa Azam Compex Chamazi umepita vigezo vyote vinavyohitajika na CAF “ku-host” mashindano yakimataifa hivyo kuanzia tarehe ya leo, uwanja huu unaruhusiwa “ku-host” mech za CAF
Bwana Khaled ameandika katika taarifa yake ya barua pepe kwenda TFF na Azam FC kuwa CAF ilimtuma mkaguziwake toka nchini Zimbabwe Bwana Wilfried Mukuna kuja kukagua uwanja huu. Bwana Mukuna aliwasilisha ripotiCAF iliyopelekea shirikisho hilo kutoa kibali kwa Azam FC na TFF kuruhusiwa kuutumia uwanja huu kwa mechizinazoandaliwa na CAF
Uongozi wa Azam FC unatoa shukrani kwa mkaguzi wa CAF Bwana Mukuna, Uongozi wa TFF chini ya Rais JamalMalinzi, na uongozi wa CAF Cairo Misri hasa Bwana Khaled Nasser kwa kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa uwazi nauweledi wa hali ya juu uliopelekea uwanja wetu kupata kibali cha kutumika kwenye michezo ya kimataifa.
Azam FC ingependa kuwataarifu wapenzi wake kuwa kuanzia msimu huu mechi zake za CAF zitachezwa AzamComplex Chamazi
http://www.youtube.com/watch?v=Ka_rNcBUgLo&feature=youtu.be
Chanzo:http://azamfc.co.tz
