NEWS

26 Machi 2014

Video: Victoria Kimani azungumzia imani yake na uwepo wa Freemason kwenye muziki wa Kenya

Story za Freemason zinaweza kuwa zimewachosha baadhi ya watu hivi sasa au wengine wanaweza kuzichukulia kama story zilizowahi kuwa maarufu, lakini kwa wengine bado hiki ni kitu cha kukifahamu hasa kuhusu uhusiano wake na watu maarufu.

Huko Kenya wasanii wengi walishawahi kuwekwa kwenye orodha ya watu wanaoaminika kuwa wanapata mafanikio kupitia nguvu za freemason kama ilivyokuwa kwa Tanzania huku mzizi wa yote ukianzia Marekani kwa wasanii wakubwa. Imani ambayo ni ‘tata’ kuthibisha.




Victoria Kimani, mwimbaji aliye chini ya usimamizi wa Chocolate City yenye makao makuu nchini Nigeria ameeleza kile anachoamini kuhusu uwepo wa freemason au Illuminati kwenye muziki muziki wa Kenya na imani yake kuhusu suala hilo.

“Ngoja niwaambie kitu, sidhani kama kuna kitu kama Illuminati au vyovyote vile ilivyo. Sidhani watakuja Kenya na kuwachukua wasanii wetu kwa sababu hatuna hata twitter verification. Hatuna hata video za nyimbo zilizohit zaidi ya milioni kwenye YouTube. Kwa hiyo sidhani kama niko kule lakini ninawa-apreciate kwa kunifikiria kwenye fikra zenu za timu ya illuminate. Mimi sio sehemu ya shirika ama jamii yoyote ya ‘secret society’.” Victoria Kimani ameuambia mtandao wa Ghafla wa Kenya.

Ameongeza kuwa yeye ni mwanamuziki ambaye yuko chini ya Chocolate City ambao wana imani ya Kikristo na endapo akijaribu kufanya kitu kama hicho wangemzingua.

Hata hivyo kwa pointi ya twitter Verificatio, wiki hii Victoria Kimani alikuwa verified na Twitter na kuwa mmiliki halali wa akaunti yake.

Mtazame akiongea hapa chini..!