NEWS

18 Aprili 2014

Ben Pol aeleza jinsi anavyoichukulia show atakayofanya Ujerumani mwezi huu


Mwimbaji wa R&B Tanzania, Ben Pol anatarajia kufanya show Munich, Ujerumani mwezi huu mwishoni ikiwa ni show yake ya kwanza kufanya nje ya nchi za jumuia ya Afrika Mashariki.

Mkali huyo wa Unanichora ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa hiyo ni ishara kubwa kwake na inaonesha kuwa sauti yake inasikika mbali.



“Kwangu mimi naizungumzia kama...sasa sauti yangu inasikika. Mimi naitafsiri ni kitendo cha sauti kusikika kwa sasa. Kwa sababu mimi sikumpigia mtu simu Ujerumani kumwambia ‘bana niandalie show au nini’. Nimekaa tu home napigiwa simu ‘bana hapa Munich Ujerumani tunataka kufanya show tarehe 30 tunaomba uje kuperform. Unawapenzi wengi, watu wanapenda nyimbo zako watu wanapenda nyimbo zako tunaomba uje kuperform’.” Amesema Ben Pol.

Mwimbaji huyo amesisitiza kuwa kupigiwa simu na mtu usiyemfahamu na anatoka nchi ambayo hakuitegemea inamaanisha kuwa kuna watu wengi duniani ambao wanafuatilia muziki wake hata kwa njia ya mtandao.

Ameongeza kuwa amewahi kupokea simu zashow kutoka nchi mbalimbali lakini walikuwa hawaelewani kimaslahi.

“Nimewahi kuzungumza na mtu wa Canada mwaka jana, nimewahi kuzungumza na mtu wa India mwaka jana lakini maslahi tu ndio kitu ambacho nilikuwa nasimamia na ndio hicho ambacho kilikuwa kinafanya nisisafiri muda wote. Lakini hawa jamaa wa Munich tumeongea vizuri, tumefikia muafaka na tumeshasaini mikataba na kila kitu kwa hiyo ni kwamba deal iko sawa, ina maslahi lakini pia ni exposure.”