‘Team Ben Pol is gonna be perfoming in München on 30th April 2014 #Twendesasa #Ready???’, hiyo ni status ya Ben Pol kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Ben Pol ambaye ameachia album yake mpya siku chache zilizopita online, ameiambia Bongo 5 kuwa show hiyo ya Ujerumani ndio ya kwanza ya kimataifa kuwahi kuipata, japo atakapokuwa huko anatarajia kufanya show zingine katika miji iliyoko karibu na anakoenda japo kwasasa hiyo ya Munchen ndiyo iliyothibitishwa.
Ameongeza kuwa waandaaji wa show hiyo walimtafuta takribani miezi mitatu iliyopita na wakawa bado hawajafikia makubaliano hadi kipindi hiki.