NEWS

18 Aprili 2014

Picha: Penny apata Mchongo mnono wa Kuigiza filamu, Jay B ndani

Penny Mungilwa anafuata nyayo za mpinzani wake Wema Sepetu kwenye filamu? Huenda ikawa hivyo sababu ni nini anaweza kukifanya akikaa meza moja na CEO wa Jerusalem Film Company, Jacob Stephen aka JB?


Penny na JB wakizungumza biashara na raia wa kigeni

Hata hivyo sio JB pekee anayehusika katika mchongo huo, kuna watu wanaonekana kuwa ni raia wa kigeni (ama Watanzania wengi asili ya mataifa mengine) wanaonekana kuamua kuwekeza kwa mastaa hao katika mradi ambao bado haujajulikana

Hapa wakiwa katika mkutano wa biashara

“Something very big is coming. Taking things to the next level. Strictly business…stay tuned,” ameandika JB kwenye akaunti yake ya Instagram.

Penny (wa pili kutoka kushoto), wait a minute… huo mkono alioubusu ni wa nani?

Naye Penny aliandika: Money making moments… Cc @jerusalemfilmco God is good.”