Rapper wa Marekani, Andre Johnson aliyejaribu kujiua kwa kujikata uume wake aliwashangaza wengi kwa kuwa kitendo hicho sio cha kawaida na wengi walitaka kufahamu sababu hasa iliyompelekea kufanya jaribio hilo.
Kwa mujibu wa E! News, chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa rapper huyo alitumia madawa hatari ya PCP ambayo yanajulikana kama Phencylidine au Angel Dust kabla ya kufanya tukio hilo na kujaribu kujirusha kutoka kwenye balcony baada ya polisi kufika na kumuomba ashuke aongee nao.
PCP yanatajwa kuwa moja kati ya madawa ya kulevya hatari zaidi na humfanya mtu kuwa na hasira na kufanya uharibifu na hupelekea watu kujifanyia mambo ya hatari zaidi.
Japokuwa rapper huyo alilkubali ombi la polisi hao, alijiachia ghafla hadi chini. Polisi walipoingia ndani ya nyumba walikuta kipande cha sehemu ya uume wa rapper huyo.
Kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo, alikimbizwa hospitalini ambapo alipewa huduma.
Hata hivyo, madaktari walishindwa kabisa kuunganisha uume wake.
19 Aprili 2014
Home
Burudani
Ripoti: Rapper wa Kundi la Wu Tang aliyejaribu kujiua kwa kujikata uume alikuwa ametumia madawa hatari 'PCP'